Former Chairman of the Main Opposition Party in Tanzania CHADEMA, Former Leader of the Opposition in Tanzania Parliament & Former Chairman of DUA.

Tanzania
Joined September 2015
Tembelea Kurasa zangu rasmi kwenye Mitandao ya kijamii.
Nimesoma neno la leo katika Kalenda ya KKKT kwenye Biblia kutoka Kitabu cha Yakobo 3 : 13 - 18. Limenirutubisha. Natamani nanyi mrutubishwe nalo. "Je, ni nani mwenye hekima na akili miongoni mwenu? Basi, aoneshe jambo hilo kwa mwenendo wake mzuri na kwa matendo yake mema yanayofanyika kwa unyenyekevu na hekima. Lakini ikiwa mioyo yenu imejaa wivu, chuki na ubinafsi, basi, msijisifu na kusema uongo dhidi ya ukweli. Hekima ya namna hiyo haitoki juu mbinguni; hekima hiyo ni ya ulimwengu, na ya kidunia, tena ni ya kishetani. Maana popote palipo na wivu na ubinafsi, hapo pana fujo na kila aina ya uovu. Lakini hekima itokayo juu mbinguni, kwanza ni safi; inapenda amani, upole na huwajali watu; imejaa huruma na huzaa matunda ya matendo mema; haina ubaguzi wala unafiki. Uadilifu ni mazao ya mbegu ambazo wapenda amani hupanda katika amani."
Nimepokea kwa mikono miwili maamuzi ya uchaguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama chetu CHADEMA uliohitimishwa leo asubuhi 22 Januari 2025. Nampongeza Mhe. Tundu Lissu na wenzake kwa kuaminiwa kutwikwa jukumu la Uongozi wa Chama. Nawatakia kila la kheri katika kukipeleka mbele Chama chetu.
Kwa viongozi wote wa Baraza la Wazee na Baraza la Vijana waliochaguliwa, hongereni kwa ushindi wenu! Bidii yenu katika harakati zetu imekuwa msingi wa mafanikio haya, inayowapa fursa ya kuwa viongozi wa kuonyesha njia kwa wengine katika kuongoza Baraza lenu. Kwa wale ambao hawakushinda mara hii, juhudi zenu zina thamani kubwa kwetu na mnabaki kuwa nguzo muhimu katika safari yetu. Tunapoangalia mbele kuelekea uchaguzi wa ndani wa Baraza la Wanawake, nawatakia kina mama wetu heri ya kufanikiwa na wepesi katika kukamilisha jukumu hili muhimu. Kumbukeni, we are Stronger Together katika kufanikisha harakati zetu za kutafuta Tanzania bora, na sasa zaidi kuliko wakati wowote, tunahitajiana. Tuendelee kujenga chama chetu kwa umoja, upendo na moyo wa ujasiri, ili pamoja, tuweze kufikia ndoto zetu. #ChademaMkutanoMkuu2025 #ChademaNationalConvention
Leo ni siku muhimu sana kwa Chadema tunapofanya uchaguzi wetu wa ndani kwa ajili ya Mabaraza ya Wazee na Vijana. Napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza wagombea wote wanaoshiriki. Kila mmoja wenu ni wa thamani kwetu katika kupigania maono ya chama chetu. Katika safari yetu hii, hebu tukumbuke kwamba uchaguzi huu ni zaidi ya nafasi; ni kuhusu kuunda mustakabali mzuri kwa Chadema na kwa Taifa letu. Sote tuna jukumu la kuilinda taasisi yetu na kuhakikisha tunamaliza hatua hii tukiwa imara zaidi. Ninawahimiza wanachama na wafuasi wote kufuatilia mchakato huu wa kidemokrasia ndani ya Chama chao. Pamoja, tukiwa na umoja, tutaweza kufanikisha mambo makubwa. Tunaposhirikiana, tunaweza kujenga Chadema yenye nguvu zaidi, kwa sababu yeyote atakae chaguliwa, Chadema imeshinda! Mungu atutangulie katika safari hii! #ChademaMkutanoMkuu2025
LIVE : FREEMAN MBOWE APOKEA UGENI NYUMBANI WA VIOGOZI NA WANACHAMA KUTOKA TANZANIA NZIMA x.com/i/broadcasts/1YqxovQDe…
LIVE : FREEMAN MBOWE APOKEA UGENI NYUMBANI WA VIOGOZI NA WANACHAMA KUTOKA TANZANIA NZIMA x.com/i/broadcasts/1ypJdpQdq…
LIVE : FREEMAN MBOWE APOKEA UGENI NYUMBANI WA VIOGOZI NA WANACHAMA KUTOKA TANZANIA NZIMA x.com/i/broadcasts/1YqKDkEok…
As the polling stations in the Local Government elections closes, the nation once again witnesses blatant and shameful misconduct by government authorities working collectively to shamelessly steal the election in favour of CCM and its candidates, even at the expense of Tanzanian lives. We strongly condemn the killings and injuries inflicted on our candidates, leaders, and members, including: 1. Steven Chalamila, from Tunduma Constituency, Songwe Region who was brutally attacked and hacked to death. 2. Modestus Timbisimilwa, a candidate for the Ulongoni A Street Committee in Gongolamboto Ward, Ukonga Constituency, Dar es Salaam, who was shot and killed by police while attempting to prevent the smuggle-in of fraudulent votes at a polling station. 3. George Juma Mohammed, from the Stand Hamlet, Mkwese Ward, Manyoni Constituency in Singida Region, who was attacked at his residence by known police officers and fatally shot. Additionally, we have received numerous reports of injuries, arrests, and detentions of our leaders, candidates, and supporters across the country as they sought to intercept and prevent the introduction of fraudulent ballots intended to favor CCM candidates. We demand the immediate and unconditional release of those detained. Our party continues to gather information and will issue an official statement once the process is complete. The ongoing actions bear the full endorsement and blessings of @SuluhuSamia and her government... the nation is effectively on "autopilot," where individuals act with impunity in their respective areas, shielded by Regulation 49 of the Local Government Election Regulations. This regulation states, and I quote: "Returning Officer, Assistant Returning Officer, Polling Station Supervisor, A Members of Appeal Committee, or any public servant involved in the election process shall not be held criminally, civilly, or administratively liable for any act or omission or commission committed in good faith while performing their duties under these Regulations." Indeed, our nation is in mourning yet again!
79
383
22
1,167
Tunapofunga vituo vya kupiga kura kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Taifa limeendelea kushuhudia tena ubaradhuli wa wazi na wa aibu toka kwa mamlaka zote za Serikali kushirikiana kuipatia CCM na wagombea wake ushindi wa aibu hata kwa gharama za maisha ya Watanzania. Tunalaani mauaji na kujeruhiwa kwa wagombea, viongozi na wanachama wetu mbalimbali wakiwemo: 1) Steven Chalamila wa Jimbo la Tunduma aliyevamiwa na kukatwakatwa mapanga kikatili hadi umauti kumkuta. 2) Modestus Timbisimilwa, Mgombea nafasi ya Ujumbe wa Serikali ya Mtaa wa Ulongoni A, Kata ya Gongolamboto, Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam aliyeuwawa na askari kwa kupigwa risasi wakati wa purukushani za kuzuia kura bandia na batili kuingizwa kituo cha kupiga kura. 3)George Juma Mohammed wa Kitongoji cha Stand Kata ya Mkwese Jimbo la Manyoni Mkoani Singida aliyevamiwa nyumbani kwake na watu waliofahamika kuwa askari na kumpiga risasi iliyomsababishia umauti. Aidha, tuna taarifa kadhaa za kujeruhiwa na kukamatwa na Polisi viongozi, wagombea, wanachama na wapenzi wetu maeneo mbalimbali ya nchi walipokuwa wakijitahidi kukamata na kuzuia kuingizwa vituoni kura bandia na batili zilizopigwa tayari kuwabeba wagombea wa CCM. Tunataka watu wetu hawa waachiwe haraka na bila masharti yeyote. Tunaendelea kuwasiliana na Chama kitatoa tamko rasmi zoezi hili likikamilika. Tunaamini kinachofanyika kina maagizo na baraka zote za @SuluhuSamia na Serikali yake na au nchi iko kwenye "autopilot" na yeyote katika eneo lake ana mamlaka ya kunajisi uchaguzi anavyotaka kwani tayari wamepewa kinga na Kanuni ya 49 ya Kanuni za Uchaguzi wa Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Ngazi ya Vijiji, Vitongoji na Mitaa inayosema, nanukuu: "Msimamizi wa Uchaguzi, Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi, Msimamizi wa Kituo, Wajumbe wa Kamati ya Rufani au mtumishi yeyote wa Umma aliyehusika na usimamizi wa uchaguzi hatowajibika kwa Jinai au Madai au kuchukuliwa kwa hatua za kinidhamu au za kiutawala kwa jambo lolote alilolifanya au kuacha kulifanya kwa nia njema wakati wa kutekeleza majukumu yake chini ya Kanuni hizi". Mwisho wa kunukuu. Hakika Taifa lina Msiba mwingine!!
Taifa linaendelea kushuhudia kwa njia mbalimbali ubakaji mkubwa wa demokrasia kwenye uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji. Wasimamizi wa "uchafuzi" huu wamekiuka kwa kiwango kikubwa hata kanuni na miongozo mibovu iliyotengenezwa kwa makusudi na hivyo kuweka mazingira ya ushindani usiyo wa haki. Madhara ya ubatili huu ni kuendelea kukosekana haki, Uhuru na demokrasia ya kweli katika ngazi ya chini zaidi na ya kwanza katika Utawala wa nchi, kunakomgusa kila mwananchi. @SamiaSuluhuHassan, Serikali na Chama chako mmeshauriwa kwa kila njia lakini hamjaonyesha chembe ya kujali haki za wananchi kwenye hili. Watanzania wote tunapaswa kutambua wajibu wa kukomesha uporaji wa haki katika uchaguzi huu hatimaye uko mikononi mwetu kila mmoja kwa eneo lake. Kwa namna ileile mnavyokosa amani katika mchakato huu, wahusika wachakachuaji wanapaswa nao kuishi kwa hofu na kukosa amani hadi pale watakaposimama katika haki kwa wote. Wananchi wasilaumiwe pale watakapochukua hatua kudai haki zao za msingi kwenye hili.
Wanaokusudia kuandamana wana hasira na wataandamana. Wanavyojiandaa kutuua na sisi tunajiandaa kufa.
Tukutane Dar Es Salaam, Jumatatu Septemba 23, 2024.
Hongera kwa @jwtz_tz kwa kutimiza miaka 60 ya kujitolea na kuhudumia taifa letu. Juhudi zenu za kulinda na kutetea Tanzania ndani na nje ya nchi ni ufahari kwa watu wote. Tunawaomba muendelee  kuwa mahiri na wathubutu katika kulinda misingi ya Katiba yetu na Watanzania wote kwa haki na usawa. Asanteni.
58
249
2
1,251
Hili ni shambulio lingine la kizushi na chuki dhidi ya Chadema na viongozi wake. Ni mkakati wa makusudi wa @tanpol wa kutafuta kisingizio cha kukamata na kutesa Wanachadema kwa taarifa toka vyanzo vya uongo. Waeleze hicho kikao cha Zoom kilifanywa na akina nani na kilikuwa na wajumbe gani!? Pamoja na @ChademaTz kutokufanya kikao kinachodaiwa, @tanpol itambue na kuheshimu haki ya makundi mengine ya kijamii kujadili #utekaji nchini. Aidha, tuhuma hizi ni mkakati wa kukwepa kuueleza Umma walipo Viongozi wa @ChademaTz @DeonisKipanya @DEUSDEDITHSOKA @JacobMlay @Mbise. @SuluhuSamia elekeza vyombo vyako vitueleze walipo vijana hawa na wengine wengi wanaoendelea kupotea nchi nzima. Utekaji ni uhalifu na kamwe hauwezi kuwa mkakati wa kulinda amani ya nchi.
LIVE : CHADEMA WANAZUNGUMZA NA WANAHABARI, TAMKO ZITO KUHUSU KUKAMATAWA KWA VIOGOZI NA WANACHAMA x.com/i/broadcasts/1ZkKzRavd…
5
95
1
458
Tunalaani vikali Jeshi la Polisi kukamata Viongozi wetu Wakuu wa Chama ikiwemo Viongozi wa Baraza la Vijana wa Chadema, BAVICHA. Aidha, tunalaani mkakati wa Msajili wa Vyama vya Siasa kwa kushirikiana na Polisi kuzuia kongamano la Bavicha katika kuazimisha siku ya vijana duniani hapo kesho j'tatu 12 Agosti. Tunadai kuachiwa haraka na bila masharti Viongozi, Wanachama na wapenzi wetu wote waliokamatwa maeneo mbalimbali ya nchi. Chama kinafuafilia kwa makini yanayoendelea na na kitaendelea kuuhabarisha Umma kila linalojiri hatua kwa hatua.