AMEPOTEA AMEPOTEA AMEPOTEA
Wadau Habari za usiku?
Nimepokea taarifa usiku huu kutoka kijijini Kishanje, Bugabo Bukoba, akitaarifu kutekwa kwa kijana Danstan Daudi Mutajura (pichani juu) anayefanya kazi Jijini Dar es Salaam.
Dastan ametekwa leo majira ya saa 4 asubuhi maeneo ya Sigara, TANESCO, Buza Jijini Dar es Salaam wakati akienda kazini kwake akitokea nyumbani kwake eneo la Kitunda, Jijini Dar es Salaam.
Dastan ametekwa na *WATU WASIOJUKIKANA* baada ya gari alilokuwa akiendesha (T.109 DYV) aina ya Mercedes Benz C300 kuzuiwa kwa mbele na gari la watekaji.
Baadaye gari la Danstan liliokotwa na kupelekwa Kituo cha Kidogo cha Polisi cha Buza na kuandikishwa kama *MALI YA KUOKOTWA* RB NO. BZA/RB/53/2025
Madereva wa bodaboda walioshugudia tukio hilo wamesema Danstan alinyofolewa kutoka kwenye gari lake na kufungwa Kitambaa usoni akilalamika kuwa alikuwa akitekwa.
Tafadhali sambaza taarifa hizi katika mitandao yote.
Simu yake +255 769 002 700 akipigwa haipatikani/haiko hewani.
Tunaendelea kufuatilia taarifa za Danstan.