TANZANIA KILLING ITS BABIES
Hadi sasa Watawala wanajizima data juu ya Mauaji ya Halaiki ya Wananchi. Wanaongelea Uhalifu, Vurugu, Uvunjifu wa Amani na Uharibifu wa Mali ila hawataki kuwajibika kwa kile kilichofanywa kwa AMRI ZAO., ambacho ni MAUAJI.
Kibaya zaidi wana SHIFT BLAME, GASLIGHT, COVER UP, JUSTIFY & SCAPEGOATING! Sasa wana waangushia JUMBA BOVU the VOICELESS & HOPELESS KIDS, na Politicians (hasa wa CHADEMA) kuwa ndio wamehamasisha fujo, na kufanya UHAINI (TREASON).
Kwanza it is “laughable & preposterous” kuwapa kesi za “Uhaini” watu walioandamana. Uhaini ni kosa la kutaka KUIPINDUA SERIKALI kinyume na utaratibu wa kikatiba, au kutoa “SIRI ZA NCHI” kwa Maadui wake.
Kweli NIFFER kuwaambia watu wanunue Barakoa kujiepusha na Teargas ni Uhaini? Au Watoto kuandamana wakisema “HATUTAKI CCM” ni Uhaini?
Kuandamana ni CONSTITUTIONAL RIGHT
Kuwa na Maoni Mbadala ni DEMOCRATIC na CONSTITUTIONAL RIGHT
Uhuru wa Kujielezea ni HUMAN RIGHT
Haki ya kutonyanyaswa na kuteswa (hata ukiwa mhalifu) ni HUMAN RIGHT
Kukataa Viongozi Unaoona Hawakufai ni DEMOCRATIC RIGHT
Kuikosoa Serikali ni DEMOCRATIC RIGHT
Kuwa na Uhuru wa Kuishi na kutouwawa ni HUMAN RIGHTS
“We, The People of Tanzanian are HUMANS led by A CONSTITUTION that is DEMOCRATIC”. Infact, Watawala ambao wanafanya maamuzi kinyume na Katiba, hao ndio WAHAINI.
Mmeua Waandamanaji. Mka impose “short notice” Curfew na ku-cripple Maisha yao ya kiuchumi. Kisha mkawafata majumbani na kuanza kuwaua kwa silaha za kivita! Mkawakatia Internet na Mawasiliano, na Uhuru wa kwenda kujitafutia Riziki; kufa njaa. Na sasa wote mliowakamata, mnawabambikia kesi za Uhaini ambazo adhabu yake ni KIFO…
Watoto wa Kimaskini, wasio na fursa, waliosahaulika na kudharaulika, aka THE DISENFRANCHISED, mmewaua kwa kuwakosesha “MATUMAINI YA KESHO YAO”. Walivyoandamana Kikatiba mmewaua kwa “SILAHA ZA MOTO”
And now waliobakia mnataka kuwaua kwa “KESI ZA UHAINI KWA ADHABU YA KIFO”
While other nations protect its kids, build their capacity, empower them with education & tools, integrate them into the work systems & think tanks, TANZANIA IS DISENFRANCHISING THEM, and yes… KILLING THEM
The Leader